Dodoma FM

Stakabadhi ghalani kujenga imani kwa wakulima

27 January 2026, 6:32 pm

Picha ni Naibu waziri wa Viwanda na Biashara Mh. Dennis Londo.Picha na Mariam Kasawa.

Maadhimisho ya miaka ishirini yatafanyika mwezi wa 4,2026 , ambapo watashirikisha wadau waliokuwa wakifanya kazi pamoja na kuwapa elimu wanafunzi na wakulima kuhusu mfumo huo.

Na Mariam Kasawa.
Naibu waziri wa Viwanda na Biashara Mh. Dennis Londo, amesema kuwa ujio mpya wa stakabadhi za ghala unawakumbusha wakulima changamoto walizopitia kupitia vyama vyao vya ushirika.
‎Ameyasema hayo wakati wa Uzinduzi wa Mfumo na kuazimisha Miaka 20 ya Kuimarisha Biashara ya Kilimo Tanzania Kupitia Mfumo wa Stakabadhi za Ghala.

Mh. Londo amesema wakulima wanapovuna na kupeleka mazao ghalani, wanategemea malipo mara moja kwa sababu changamoto zao ni kusuluhisha madeni, mikopo, ada za watoto, na huduma za afya hata hivyo, wakulima hawa wanaona kama wanakopesha mazao yao kutokana na kucheleweshwa malipo, hali inayotokana na ukosefu wa imani.

Sauti ya Mh. Dennis Londo,

‎Awali akizungumza Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala, Asangye Bangu, amesema kuwa mfumo wa stakabadhi za ghala umeleta mafanikio makubwa katika miaka ishirini, ikiwemo kuboresha bei, kuongeza uzalishaji na ubora wa bidhaa.

Aidha, amebainisha kuwa bidhaa kumi na nane sasa zinatekelezwa kupitia mfumo huu na mpango wa kuongeza bidhaa zisizo za kilimo kama mifugo, uvuvi, na madini unatekelezwa.

Sauti ya Asangye Bangu.