Dodoma FM
Dodoma FM
26 January 2026, 5:11 pm

Pamoja serikali kujitahidi kutoa Elimu kupitia vyombo mbalimbali lakin Bado wilaya ya Mpwapwa inakabiliwa na changamoto za wazazi au walezi kuwatoa watoto wao Kwenda mikoa ya mbali Kwa kazi za ndani au kuchunga mifugo.
Na Steven Noel.
Hatimae serikali wilaya Mpwapwa imeingilia kati sakata la mtoto Rajabu Sulemani (13)wa Mpwapwa alieokotwa jijini Dar-es- salaam Katika mazingira magumu na kufanikisha kumrudisha Nyumbani na kukabidhiwa Kwa wazazi wake .
Akiongea na vyombo vya habari Afisa ustawi wilaya ya Mpwapwa Bi Rose Sichilima amesema kuwa kupitia mitandao ya kijamii alipata taarifa za mtoto wa Mpwapwa alitangazwa na vyombo vya clouds fm kuwa mtoto mdogo alieokotwa Polini na mama msamalia ndipo ilipowalazimu kuchukua hatua za kilifuatilia suala Hilo Kwa kina na hatimae kufanikiwa kumrudisha kijana huyo mikononi mwa wazazi wake.
Akiongea mama aliye muokota mtoto huyo Bi Mwamvita Mwanja amesema Katika shughuli zake alimuona mtoto huyo akiwa Porini amechoka na Yuko Katika Hali mbaya ya kiafya na kimuonekano na ndioo alichukua jukumu la kuwapigia Simu clouds Ili wamtangaze Kwa lengo wapatikane wazazi wake.
Video 2. Bi Mwavita mwanja
Mama mzazi wa mtoto huyo Bi Asifiwe Ernest Alisema baada ya kutokea mgogoro wa kidamilia walitengana na mzazi mwenzie huyo ndioo baba wa watoto aliwachukua watoto Kwa lengo la kukaa nao lakini nae aliwatoroka watoto na kukimbilia Tanga na kuwatelekeza watoto hao.
Kwa upande wake kaimu mkurugenzi mtendaji halmashauri ya Mpwapwa ambae pia ni Afisa maendeleo ya Jamii bwana bwana Bahati Magumula alikemea tabia baadhi ya wazazi kuwatumia watoto kama kitega uchumi na kuwakosesha Haki Yao ya kielimu.