Dodoma FM
Dodoma FM
22 January 2026, 5:44 pm

Umekuwa muendelezo wa kampeni ya Onesha Upendo inayoratibiwa na kituo cha Dodoma Media Group katika kugusa makundi mbalimbali katika jamii ambapo kwa mwaka huu wakitarajiwa kutoa msaada wa vitu mbalimbali katika kituo hicho.
Na Anwary Shabani.
Kupitia kampeni ya Onesha Upendo ya Dodoma Media Group inayotarajiwa kufanyika Febuari 14, 2026 katika kituo watoto yatima Qadiria kilichopo Ndachi Dodoma wamewaalika wadau wengine kuungana nao katika tukio hilo.
Afisa Masoko kutoka Dodoma Media Group Valeria Kamaleki amesema onesha upendo kwa mwaka huu inatarajia kutoa mahitaji mbalimbali ikiwemo vyakula na mahitaji mengine muhimu kama anavyobainisha.
Kwa upande wake, Peter Lugumi, ambaye ni Mkurugenzi wa THE BSL INVESTMENT COMPANY LIMITED na mfanyabiashara katika Jiji la Dodoma, amewataka wadau mbalimbali kujitokeza kwa moyo wa hiari kutoa chochote walichonacho kwa ajili ya watoto hao.
Aidha Valeria ameweka wazi mfumo sahihi wa kupokea misaada hiyo kwa kueleza kuwa wananchi wanaweza kufikisha misaada yao moja kwa moja au kuwasiliana na waandaaji wa zoezi hilo.