Dodoma FM
Dodoma FM
22 January 2026, 5:14 pm

Mradi huo unawezeshwa na Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo.
Na Lilian Leopold.
Kupitia mradi wa Tanzania Youth and Smallholder Productivity Upgrade (TYSPU), jumla ya mashamba darasa nane ya zao la alizeti yanayosimamiwa na Halmashauri ya Jiji la Dodoma yamenufaika na mbegu bora, mbolea pamoja na viuatilifu, hatua inayolenga kuongeza uzalishaji na kuhakikisha wakulima wanafanya kilimo chenye tija na chenye tija zaidi.
Mradi huo unawezeshwa na Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo, kwa lengo la kuboresha upatikanaji wa pembejeo za kilimo, kuongeza maarifa kwa wakulima pamoja na kuimarisha uzalishaji wa mazao ya kimkakati ikiwemo alizeti.

Akizungumza kuhusu utekelezaji wa mradi huo, maafisa kilimo kutoka Jiji la Dodoma akiwemo Athumani Mpanda na Emmanuel Mayyo wameeleza kuwa mashamba darasa hayo yanatumika kama vituo vya mafunzo kwa wakulima, ambapo wanapatiwa elimu ya vitendo juu ya matumizi sahihi ya mbegu bora, mbolea na viuatilifu ili kuongeza tija na ubora wa mazao.