Dodoma FM

Kaimu Mkurugenzi Bodi ya Waandishi afanya ziara Dodoma

21 January 2026, 3:54 pm

Picha ni wahariri na waandishi wa habari wa vyombo vya habari wakizungumza na Mwenyekiti wa Bodi ya Ithibati Ndg. Tido Mhando. Picha na Okuly Blog.

Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari inalenga kuhakikisha waandishi wanatimiza kanuni, sheria na maadili ya uandishi wa habari, pamoja na kulinda hadhi na heshima yao katika jamii.

Na Mariam Kasawa.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari, Bw. Patric Kipangula, Januari 20, 2026, alifanya ziara ya kutembelea baadhi ya vituo vya redio na runinga jijini Dodoma.

Lengo la ziara hiyo ni kukagua utekelezaji wa sheria na kanuni za utumishi, ikiwemo kuzingatia matumizi ya vitambulisho vya Waandishi wa Habari vilivyothibitishwa na bodi hiyo.

Aidha, Bw. Kipangula ametoa maelekezo kwa wamiliki wote wa vyombo vya habari nchini kuhakikisha wanatekeleza maelekezo yanayotolewa na Viongozi, pamoja na kuzingatia mazingira bora ya kazi na maslahi ya Watumishi wao.

Sauti ya Patric Kipangula.