Dodoma FM

Ukame waathiri mifugo Kiteto, wafugaji waomba msaada

21 January 2026, 3:29 pm

Picha ni baadhi ya mifugo iliyokufa wilayani Kiteto mkoani Manyara. Picha na Kitana Hamis.

Hali hiyo imewalazimu wafugaji kuanza kutumia njia mbadala ili kunusuru mifugo yao, huku wakikabiliwa na changamoto ya ukosefu wa pumba na malisho.

Na Kitana Hamis.

Ukame unaoendelea wilayani Kiteto mkoani Manyara umeendelea kuwaathiri wafugaji, baada ya mifugo kukosa chakula na maji, hali iliyosababisha baadhi ya mifugo kufa.

Mfugaji mmoja wa kijiji cha Partimbo amesema kwa sasa analazimika kuchukua gunia la mahindi na kwenda kusaga, ili mabaki ya pumba anayoyapata ayatumie kama chakula cha mifugo yake, baada ya kushindwa kupata pumba sokoni.

Amesema hali hiyo ni ngumu, lakini hana njia nyingine zaidi ya hiyo ili kuhakikisha mifugo yake haiendelei kufa kutokana na njaa.

Picha ni baadhi ya mifugo iliyokufa wilayani Kiteto mkoani Manyara. Picha na Kitana Hamis.

Kwa upande mwingine, wafugaji wameeleza kuwepo kwa changamoto ya baadhi ya watu wanaodaiwa kufanya utapeli katika uuzaji wa pumba, hali inayozidi kuwaumiza wafugaji waliokwishaathirika na ukame.

Akizungumza kuhusu hali hiyo, Mwenyekiti wa Kijiji cha Partimbo ameiomba Serikali pamoja na wadau mbalimbali kuingilia kati kwa haraka kwa kutoa chakula cha mifugo na kudhibiti vitendo vya utapeli, akisema mifugo ni chanzo kikuu cha maisha ya wananchi wa eneo hilo.