Dodoma FM
Dodoma FM
19 January 2026, 3:58 pm

Milioni 36 ya wafanyakazi Tanzania, milioni 25.95 sawa na 71.8% wanafanya kazi katika sekta isiyo rasmi.
Na Steven Noel.
Wafanyabiashara soko dogo la Vighawe, wilaya ya Mpwampwa jijini Dodoma wameiomba serikali kuwaboresha miundombinu ya soko na kuwawezesha upatikanaji wa mikopo nafuu ili kuwasaidia kukuza mitaji yao na kuinua kipato chao pamoja na uchumi wa familia na taifa kwa ujumla.
Kulingana na ripoti ya uchambuzi wa soko la ajira mwaka 2025, kati ya takribani milioni 36 ya wafanyakazi Tanzania, milioni 25.95 sawa na 71.8% wanafanya kazi katika sekta isiyo rasmi na milioni 10.17 sawa na 28.2% wanafanya kazi katika sekta rasmi.
Katika sekta isiyo rasmi, biashara ndogondogo na uuzaji wa bidhaa sokoni zimetajwa kuchangia kwa kiasi kikubwa katika kutoa ajira hapa nchini, huku vijana na wanawake wakionekana kutegemea kazi hizi.
Hata hivyo pamoja na mchango mkubwa wa sekta hiyo katika uchumi wa wananchi, wafanyabiashara hao wameendelea kukabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ubovu wa miundombinu ya kufanyia biashara.
Taswira ya habari imefika katika soko dogo la Ving’hawe, kwa lengo la kuzungumza na wafanyabiashara hao ili kusikiliza changamoto zao.