Dodoma FM
Dodoma FM
19 January 2026, 3:09 pm

Mfumo huo unarahisisha utambuzi wa makazi, ufuatiliaji wa huduma muhimu pamoja na kuchochea maendeleo ya mijini na vijini.
Na Anwary Shaban.
Katika kuelekea kongamano la Anwani ya Makazi litakaloanza Februari 02 hadi 08 jijini Dar es salaam wananchi wametakiwa kujitokeza kwa wingi ili kupata elimu kuhusu umuhimu na matumizi sahihi ya mfumo wa anwani ya makazi.
Akizungumza na Taswira ya Habari, Afisa Ardhi kutoka Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Kitengo cha Anwani ya Makazi, Jijini Dodoma Arnold Mkude, amesema mfumo wa anwani ya makazi una mchango mkubwa katika nyanja ya kiuchumi na kijamii kwani urahisisha utoaji wa huduma za kijamii, biashara pamoja na usalama.
Aidha Mkude ameongeza kuwa mfumo huo unarahisisha utambuzi wa makazi, ufuatiliaji wa huduma muhimu pamoja na kuchochea maendeleo ya mijini na vijini, hivyo amewataka wananchi kuhakikisha wanajisajili.
Sanjari na hayo, Mkude amehitimisha kwa kutoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki katika kongamano la Anwani ya Makazi, akisisitiza kuwa zoezi la usajili kwa wananchi wataojitokeza litafanyika bure , kwa kuwa ni haki ya kila mwananchi kupata anwani sahihi ya makazi yake.
Kongamano hilo limebebwa na kauli mbiu isemayo “ Anwani za Mkazi kwa Maendeleo ya Kijamii na Kiuchumi”.