Dodoma FM
Dodoma FM
16 January 2026, 3:05 pm

Wananchi wamesema baadhi ya kaya kijijini hapo wanaishi wazee ambao hawawezi kumudu gharama za manunuzi ya chakula cha kila siku.
Na Victor Chigwada.
Baadhi ya maeneo katika mkoa wa Dodoma yanakabiliwa na upungufu wa chakula kwa sasa licha ya msimu wa kilimo kuanza.
Miongoni mwa vijiji vinavyokabiliwa na uhaba wa chakula ni pamoja na kijiji cha Nayu kilichopo kata ya Dabalo wilayani Chamwino jijini Dodoma, wananchi wa eneo hilo wamesema janga la njaa limenza kuwa tatizo kwa baadhi ya familia kijijini hapo.
Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha Nayu Bw. Samson Noha amekiri uwepo wa uhaba wa chakula kijijini hapo, hali inayowalazimu kutafuta njia mbadala ya kuzisaidia kaya zilizoishiwa kabisa akiba ya chakula.
Noha amesema kuwa wameendelea kusaidia misaada binafsi pamoja na wadau mbalimbali waliopo kijijini hapo lengo likiwa ni kuhakikisha kila mmoja anapata chakula.