Dodoma FM

Sheria zizingatiwe ili kulinda uraia

16 January 2026, 2:40 pm

Picha ni Mrakibu  Msaidizi wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Dodoma Steven Muhina,katika kipindi cha Dodoma Live kupitia Dodoma FM. Picha na Dodoma FM.

Vile vile Mrakibu msaidizi Muhina amewataka wananchi waliopewa uraia kwa mujibu wa sheria waendelee kutii sheria pasipo kukiuka utaratibu waliopewa ili wasiweze kupoteza hadhi ya kuwa raia wa Tanzania.

Na Jerome John.

Wananchi ambao ni raia wa Tanzania wametakiwa kuheshimu hadhi ya kuwa raia kwa kutovunja sheria za nchi na kufuata taratibu na miongozo inayotolewa.

Wito huo umetolewa na Mrakibu  Msaidizi wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Dodoma Steven Muhina wakati akizungumza na Taswira ya Habari juu ya tafsiri ya urai na raia wa Tanzania.

Mrakibu Muhina amesema kuwa raia wa Tanzania ana haki zote za kuishi bila kuwa na mipaka na ana wajibu wa kuzitii sheria zote za nchi bila kuvunja misingi ya kikatiba na miongozo iliyopo.

Aidha amebainisha kuwa raia wa Tanzania ana wajibu wa kujielimisha juu ya masuala ya uraia na kutojiusisha na uvunjifu wa amani au ukiukaji wa sheria za nchi na kutoa taarifa pindi anapobaini kuwa kuna raia wa kigeni ambao hawakufuata sheria za nchi kuingia hapa nchini.

Sauti ya Steven Muhina