Dodoma FM

Serikali kuendelea kuboresha maslahi ya watumishi wa TRA

16 January 2026, 2:23 pm

Picha ni Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mcha Musa Mcha wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Kukusanya Mapato Tanzania (TAREU) jijini Dodoma. Picha na Mariam Kasawa.

Mkutano huo uliwakutanisha wadau mbalimbali kwa lengo la kuimarisha sekta ya ukusanyaji mapato nchini.

Na Mariam Kasawa.

Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mcha Musa Mcha, amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya uongozi wa mamlaka hiyo na wafanyakazi ili kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato ya serikali.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Kukusanya Mapato Tanzania (TAREU) jijini Dodoma, Mcha alibainisha kuwa TRA inathamini sana mawazo kutoka kwa wafanyakazi.

Ameeleza kuwa maoni hayo yanachangia kwa kiasi kikubwa katika,Uundaji wa sera mbalimbali, kuboresha ustawi wa wafanyakazi na Kuweka mazingira bora ya kazi ili kuchochea ufanisi.

Aidha, Naibu Kamishna huyo amekumbusha kuwa katika mwaka huu wa fedha, serikali imeanza kutekeleza maboresho ya maslahi ya watumishi kwa awamu, na kuahidi kuwa mpango huo utaendelea kutekelezwa kikamilifu.

Sauti ya Mcha Musa Mcha.
Picha ni Alex Dennis Mwenyekiti wa TAREU kwakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Kukusanya Mapato Tanzania (TAREU) jijini Dodoma. Picha na Mariam Kasawa.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa TAREU, Alex Dennis, ameeleza kuwa chama hicho kina dhamira ya kuendelea kuwasaidia wafanyabiashara ili waweze kupiga hatua. Alisisitiza kuwa watumishi wa mapato ni washirika wa wafanyabiashara na si maadui zao.

Katika mkakati wa kutatua changamoto, Dennis ametangaza kuwa Wanaendesha zoezi linaloitwa “Tax Clinic” ambalo huwapa fursa wafanyabiashara kusikilizwa huku Lengo ni kutatua changamoto mbalimbali ndogondogo zinazowakabili walipa kodi.

Sauti ya Alex Dennis.