Dodoma FM
Dodoma FM
16 January 2026, 12:50 pm

Nae Maria Manyelezi amesema pamoja na ukosefu wa chumba cha kuhifadhia maiti, pia kijiji hicho kinakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa maji safi na salama na hivyo kumpelekea kijiji hicho kukmbwa na mlipuko wa magonjwa ya mara kwa mara.
Na Steven Noel.
Wananchi wa kijiji cha Mbori wilaya ya Mpwapwa, jijini Dodoma wameiomba serikali kuwaondolea changamoto ya ukosefu wa chumba cha kuhifadhia maiti ili kuepuka kuzika miili ya ndugu zao kabla ya wakati au kutumia gharama kubwa kuhifadhi miili katika hospitali ya wilaya.
Wakizungumza mbele ya Mbunge wa Jimbo la Mpwapwa George Malima wananchi wa kijiji hicho wameiomba serikali kuwasaidia kupata chumba cha kuhifadhia maiti.
Lukas Mwakayeye ni Mwenyekiti wa kamati ya uendeshaji wa kituo cha afya Mbori amesema kufuatia changamoto hiyo huwalazimu baadhi ya ndugu kutumia gharama kubwa kupeleka kuhifadhi mwili katika hospitali ya wilaya umbali wa kilomita 20, au kuzikwa haraka haraka na hivyo kuwanyima haki ya kiimani au kiutamaduni kushidwa kuaga mwili wa mpendwa wao anapofariki.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Mpwapwa George Nathan Malima amekiri kuwepo kwa changamoto hizo akisema kuwa kwa kushirikiana na serikali wataendela kuzitatua.