Dodoma FM

Wanaume wajitokeze kuwapeleka wake zao kliniki

15 January 2026, 3:13 pm

Picha ni Mganga Mkuu wa Serikali, DK. Grace Magembe. Picha na Wizara ya Afya.

Hii ni kutokana na ushiriki wa wanaume kuwa hafifu katika masuala ya afya ya uzazi, hali inayosababisha wanawake wengi kuhudhuria kliniki peke yao bila msaada wa wenza wao, jambo linalopunguza uelewa wa pamoja kuhusu hatua muhimu za ujauzito, kujifungua na malezi ya mtoto, na hivyo kuongeza hatari za vifo vya akina mama na watoto vinavyoweza kuzuilika.

Na Steven Noel.

Wanaume wameshauriwa kujitokeza kwa wingi kuwasindikiza wake zao wajawazito kliniki ili kuongeza uelewa wa pamoja kuhusu elimu ya afya ya uzazi, kuimarisha ushirikiano ndani ya familia na kuchangia kwa kiasi kikubwa kupunguza vifo vya akina mama na watoto vinavyotokana na changamoto zinazozuilika wakati wa ujauzito na kujifungua.

Kauli hiyo imetolewa na Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Dkt. Stanley Msuya, wakati wa zoezi la uhamasishaji wa jamii, hususan akina mama, kuhusu umuhimu wa kujifungulia katika vituo vya afya ili kupata huduma salama na za kitaalamu kwa afya ya mama na mtoto.

Sauti ya Stanley Msuya.