Dodoma FM

Gunners yaachana na Juma Ikaba

15 January 2026, 11:27 am

Picha ni aliyekuwa kocha wa Gunners fc Juma Ikaba ambaye ameachana na timu hiyo kwa sasa.Picha na Gunnersfc.

Ikaba ndiye kocha alianza kukinoa kikosi cha guuners kwanzia ligi ya mkoa kisha daraja la pili na kwa sasa alikuwa akikiongoza kikosi hichi katika ligi daraja la kwanza.

Na Hamis Makila.
Kikosi cha guuners kimefikia makubaliano ya pande zote mbili ya kuachana na aliyekuwa kocha na aliyekuwa kocha wake Juma Ikaba.

Hayo yamedhibitishwa na afisa habari na mawasiliano wa kikosi hicho Chriss Mzena wakati akizungumzia maandalizi ya kikosi hicho kuelekea mchezo unaofuata wa ligi daraja la kwanza dhidi ya polisi Tanzania mchezo utakaopigwa jan17 katika dimba la ushirika moshi.

katika hatua nyingine mzena amebainisha kikosi hicho kitakuwa chini ya kocha wa muda ambaye ni Henry Nkanwa aliyewahi kuwa kocha wa zamani wa kitayocse,pamba jiji kama kocha msaidizi kishaakakinoa kikosi cha biashara united.

Ikaba ndiye kocha alianza kukinoa kikosi cha guuners kwanzia ligi ya mkoa kisha daraja la pili na kwa sasa alikuwa akikiongoza kikosi hichi katika ligi daraja la kwanza,hata hivyo kocha huyo alikiongoza kikosi hichi kwenye michezo 14 akishinda michezo 3 sare kwenye michezo 5 huku akishinda michezo 6.