Dodoma FM

Wakulima Dodoma watakiwa kujikita katika kilimo cha umwagiliaji

13 January 2026, 4:22 pm

Picha ni wakulima wa nyanya ambao wanalima kilimo cha umwagiliaji .Picha na AMDT.

Wadau wa kilimo jijini Dodoma wanasema kuwa kuwekeza katika kilimo cha umwagiliaji ni njia sahihi ya kukabiliana na changamoto ya ukame, kuongeza uzalishaji wa mazao na kuhakikisha usalama wa chakula kwa sasa na siku zijazo.

Na Anwary Shaban.
Wakulima Jijini Dodoma wametakiwa kujikita zaidi katika kilimo cha umwagiliaji ili kuongeza uzalishaji wa mazao na kuimarisha usalama wa chakula, hasa katika kipindi cha ukame kinacholikumba eneo la ukanda wa kati.

Wito huo umetolewa na Gratian Elias Mwesiga, ambaye ni Mkuu wa Divisheni ya Kilimo Jiji la Dodoma, alipokuwa akizungumza na Taswaira ya Habari kuhusu juhudi za serikali katika kuimarisha sekta ya kilimo.
Gratian Elias amesema kuwa kilimo cha umwagiliaji ni suluhisho la uhakika kwa wakulima wa Dodoma kutokana na mvua zisizotabirika, kwani kinawawezesha kulima kwa msimu wote na kuongeza mavuno, hatua itakayosaidia kuwepo kwa usalama wa chakula kwa wananchi.

Sauti ya Gratian Elias Mwesiga.

Aidha, Gratian Elias amebainisha kuwa changamoto ya ukosefu wa rasilimali fedha bado ni kikwazo kikubwa kwa wakulima wengi kuwekeza katika kilimo cha umwagiliaji. Amehimiza wakulima kujiunga na vyama vya ushirika ili waweze kupata mikopo kutoka taasisi za kifedha na kuimarisha shughuli zao za kilimo.

Sauti ya Gratian Elias Mwesiga.

Kwa upande wake, Robert Kombo, ambaye ni mmoja wa wakulima wanaojishughulisha na kilimo cha umwagiliaji jijini Dodoma, amesema kuwa kilimo hicho kimekuwa na manufaa makubwa ikiwemo kupata mavuno ya uhakika na kipato endelevu.

Sauti ya Robert Kombo