Dodoma FM

Ukosefu wa elimu ya fedha changamoto kwa vijana

13 January 2026, 1:27 pm

Picha ni mmoja wa wanufaika wa mkopo wa asilimia 10 kata ya Kizota jijini Dodoma. Picha na Dodoma FM.

Lengo la mkopo wa asilimia 10 wa halmashauri ni kusaidia vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, ili kukuza maendeleo ya kiuchumi.

Na Victor Chigwada.

Ukosefu wa  elimu ya matumizi bora ya fedha  na nidhamu ya fedha umepelekea baadhi ya vijana kushindwa kunufaika na mkopo wa asilimia 10 unaotolewa na serlikali kupitia halmashauri kwa makundi ya vijana , wanawake na watu wenye ulemavu.

Wakizungumza na taswira ya habari baadhi ya vijana wa kata ya Msamalo wilayani Chamwino  wamesema kuwa  Mikopo ya asilimia 10 imekuwa msaada kwao na pia imewaepusha na mikopo umiza ambayo walikuwa wakipeana wenyewe kwa wenyewe.

Aidha wamesema kuwa licha ya uwepo wa mikopo hiyo lakini bado wanakumbana  na adha ya kupata mikopo hiyo kwa kukosa vigezo vya kupata mikopo hiyo na wakati mwingine mikopo inatolewa Kwa vikundi vichache.

Sauti za vijana.

Afisa maendeleo wa Kata ya Msamalo Bi.Ngw’ashi Muhuri amesema kinacho waangusha vijana wengi ni kutaka kupata matokeo ya haraka wanapo pata fedha huku baadhi Yao wakianzisha vikundi wakiwa na malengo binafsi.

Sauti ya Ngw’ashi Muhuri.

Muhuri ameongeza kuwa amewahi kukutana na changamoto ya kikundi kuchukua fedha badala ya kufanya mradi wa kikundi wakagawana fedha Kila mtu na biashara yake mwisho wa siku wakashindwa kufanya marejesho

Sauti ya Ngw’ashi Muhuri.