Dodoma FM

Maafisa usafirishaji walalamikia mikataba kandamizi ya pikipiki

12 January 2026, 2:34 pm

Picha ni baadhi ya maafisa usafirishaji ( bodaboda) katika eneo la Majengo Sokoni jijini Dodoma. Picha na Dodoma FM.

Aidha wamebainisha kuwa kutokana na kukosa elimu ya kisheria ndo maana wanakumbana na mrorongo wa kukiukwa kwa makubaliano dhidi ya wamiliki wa pikipiki hizo na kujikuta wanashindwa kuzimiliki hizo pikipiki.

Na Jerome John.

Maafisa usafirishaji (boda boda) mkoani Dodoma wamelalamikia suala la mikataba ya kazi baina yao na wamiliki wa pikipiki wanazozitumia katika shughuli zao.

Boda boda hao wakizungumza na Taswira ya habari  wameelezea changamoto hiyo ni kukiuka makubaliano yao na baadhi ya wamiliki wa vyombo hivyo kwa kuongeza muda wa marejesho ya fedha  badala ya miezi 12 hadi miezi 18 na zaidi tofauti na makubaliano ya awali wanayokuwa wamekubaliana.

Sauti za maafisa usafirishaji.

Kwa upande wake Afisa Sheria Mfawidhi wa Halmashauri ya Mpwapwa Emmanuel Madelele amesema kuwa ni wakati sasa wa boda boda kuhakikisha wanaingia mikataba ya kisheria kwa kuwahusisha wataalamu wa sheria na kuweka masharti ya malipo yanayoeleweka kila upande na kukubaliana muda maalum wa mikataba hiyo.