Dodoma FM

Wazazi watakiwa kuwaandikisha watoto shule 2026

9 January 2026, 4:48 pm

Kwa mujibu wa Sheria ya Mtoto Na. 21 ya Mwaka 2009 pamoja na Sheria ya Elimu Na. 25 ya Mwaka 1978 (iliyofanyiwa marekebisho, mtoto mwenye umri wa kuanzia miaka 6 anatakiwa kuandikishwa kuanza elimu ya msingi. Ni wajibu wa mzazi au mlezi kuhakikisha mtoto anaanza na kuendelea na masomo. Picha na Blog.

Aidha mwanasheria huyo ameeleza kuwa endapo mzazi atashindwa kufanya hivyo atachukuliwa hatua stahiki na atatakiwa kueleza sababu ni zipi zilizopelekea kushindwa kwake kutimiza wajibu wake.

Na Mwandishi wetu.

Wazazi na walezi nchini wametakiwa kuhakikisha wanawaandikisha watoto shule katika kuanza muhula wa masomo wa mwaka 2026.

Akizungumza na Taswira ya habari mwanasheria kutoka kituo cha kutetea haki za watoto,ndugu Amosi Kameli amesema kuwa ni wajibu wa mzazi au mlezi kuhakikisha mtoto mwenye umri wa kuanzia miaka sita anaandikishwa kuanza elimu ya msingi kwa mujibu wa sheria ya mtoto na sheria ya elimu.

Vile vile ndugu Kameli amebainisha kuwa kama mzazi amekuwa na changamoto za kiuchumi ambazo zimepelekea ashindwe kufanya hivyo anatakiwa kutoa maelezo mapema kwa viongozi wa serikali ili mtoto huyo awezekupata msaada wa mapema na aendelee na masomo yake,sheria hizo zinawataka pia wazazi na walezi amabao wanawatoto wanaokwenda kuanza kidato cha kwanza kuzizingatia.

Sauti ya Amosi Kameli