Dodoma FM

Migodi ya Manyemba, Nayu yahitaji nishati ya umeme

9 January 2026, 4:24 pm

Wachimbaji hao wamesema ukosefu wa umeme umekuwa ukikwamisha shughuli zao za katika migodi hiyo. Picha na Gazeti la Mwananchi.

Wameongeza kuwa endapo watapatiwa huduma ya umeme katika machimbo hayo itasaidia kukuza uwekezaji na kurahisisha uchimbaji.

Na Victor Chigwada.

Wananchi wanaojishughulisha na uchimbaji wa madini aina ya dhahabu katika migodi ya Manyemba na Nayu Kata ya Dabalo Wilaya ya Chamwino wameiomba Serikali kusambaza miundombinu ya nishati ya umeme ili kurahisisha kazi ya uchimbaji.

Wakizungumza na Taswira ya habari baadhi ya wachimbaji wa madini katika migodi hiyo wamesema  kukosekana Kwa  umeme katika migodi hiyo kunapelekea uzalishaji kuwa duni kwani wachimbaji hushindwa kutumia vifaa vya kisasa katika uchimbaji.

Sauti za wachimbaji wa madini.

Nae Diwani wa Kata ya Dabalo Bw.Omary Kiguna amesema kuwa licha ya upatikanaji wa madini katika machimbo hayo ukosefu wa umeme umekuwa ukikwamisha kazi ya uchimbaji kwa kiasi kikubwa.

Sauti ya Omary Kiguna.