Dodoma FM
Dodoma FM
9 January 2026, 4:10 pm

Kwa sasa shule hiyo imezidiwa na wingi wa wanafunzi hali inayopelekea darasa moja kukaliwa na wanafunzi hadi 100.
Na Victor Chigwada.
Mrundikano wa wanafunzi katika shule ya msingi Dabalo, wilaya ya Chamwino jijini Dodoma umepelekea wanafunzi kushindwa kuwaelewa walimu wanapokuwa darasani.
Wakizungumza na Taswira ya habari wakazi wa kijiji cha Dabalo wameiomba serikali kurudisha eneo alilopewa mwekezaji akashindwa kuliendeleza ili waweze kujenga vyumba vya madarasa mengine ambayo yatapunguza mrundikano wa wanafunzi ambao unaikabili shule hiyo kwa sasa.
Bw. Omary Kiguna diwani wa Kata ya Dabalo amekiri shule hiyo kuzidiwa na wanafunzi hali inayopelekea wanafunzi wengi kurundikana katika darasa moja hivyo ameomba serikali itoe eneo hilo ili waweze kuongeza vyumba vya madarasa.
Sauti ya Omary Kiguna.