Dodoma FM
Dodoma FM
8 January 2026, 4:46 pm

Wameeleza kuwa uwazi wa mapato na matumizi yatokanayo na shughuli za uchimbaji wa madini katika mgodi wa Nholi ni jambo la msingi katika kuimarisha uwajibikaji na ushiriki wa wananchi katika masuala ya maendeleo ya kijiji.
Na Victor Chigwada.
Wakazi wa kijiji Cha Nholi wWilayani Chemba jijini Dodoma wameitaka serikali ya kijiji kuweka wazi mapato na matumizi yanayotokana na shughuli za uchimbaji wa madini katika mgodi wa Nholi kijijini hapo.
Wakizungumza na Taswira ya habari wananchi hao wamesema licha ya kijiji hicho kuingiza mapato kutokana na mgodi lakini wamekuwa na sintofahamu kwani hakuna vikao vyovyote vilivyofanyika kuhusu mapato na matumizi.
Akijibu malalamiko ya wananchi mwenyekiti wa kijiji hicho Carolina Mtuli amesema kuwa wanatarajia kuchukua hatua za ufuatiliaji kwani hapo awali kulikuwa na taarifa za ucheleweshwaji wa asilimia za kijiji kutoka halmashauri.
Hivyo taarifa kamili ataitoa pindi atakapo kufanya ufuatiliaji kwa mtendaji wa kijiji .