Dodoma FM

Umbali wa shule changamoto kwa vitongoji vya Mgokoo, Mailimbili

8 January 2026, 3:39 pm

Umbali wa shule katika maeneo hayo umepelekea baadhi ya wanafunzi kukata tamaa na kuacha shule huku wazazi wakishindwa kuchukua hatua yoyote . Picha na Dodoma City TV.

Changamoto ya umbali wa shule, inayowalazimu wanafunzi kutembea umbali mrefu na wakati mwingine kuvuka barabara, jambo linalohatarisha usalama wao na kusababisha baadhi yao kukata tamaa na kuacha shule.

Na Victor Chigwada.

Ikiwa zimesalia siku chache kabla ya shule za msingi na sekondari kuanza muhula mpya wa masomo kwa mwaka 2026 baadhi ya maeneo yamekumbwa na sintofahamu kutokana na shule kuwa mbali.

Baadhi ya maeneo yanayo kumbwa na adha ya shule kuwa mbali ni pamoja na vitongoji vya Mgokoo na Mailimbili vilivyopo Kata ya Mlowa Barabarani katika wilaya ya Chamwino jijini Dodoma .

Kwa mujibu wa sera ya elimu ya mwaka 2014 Serikali ya Tanzania katika nyakati tofauti imechukua hatua mbalimbali za kurekebisha mfumo wa elimu ili kufikia malengo ya maendeleo na kuleta matokeo tarajiwa. Kwa sababu hiyo, sera zinazoongoza elimu zimekuwa zikiboreshwa ili kukidhi malengo ya mfumo wa elimu kwa kipindi husika.

Sauti za wananchi.

Anjero Lucas Diwani wa Kata ya hiyo amesema vitongoji hivyo vinakabiliwa na kukosa huduma ya elimu Kwa ukaribu na hata wakati mwingine watoto kuvuka barabara jambo linalo hatarisha usalama wao.

Sauti ya Anjero Lucas.