Dodoma FM
Dodoma FM
7 January 2026, 3:37 pm

Ukosefu wa maji safi na salama umekuwa ukiwaathiri zaidi wanawake na watoto, kutokana na kutembea umbali mrefu kufuata huduma ya maji safi. Picha na Mzalendo.
Kutokana na ukosefu wa maji safi na salama wananchi wanakabiliwa na hatari ya kiafya kwani maji yanayotumika sio safi na salama kwa matumizi ya nyumbani.
Na Victor Chigwada.
Serikali imeombwa kutatua kero ya ukosefu wa maji safi na salama katika kijiji cha Nholi kata ya Mpalanga wilayani Chemba.
Wakizungumza na Taswira ya habari wakazi wa kijiji hicho wamesema adha hiyo imekuwa ikiwatesa zaidi wanawake kwani wanatumia muda mwingi kutafuta maji wakati mwingine hulazimika kuchimba visima kwa mikono ili kupata maji au kuchota maji yaliyotuama kwenye madimbwi ambayo si salama.
Mwenyekiti wa Kijiji Cha Nholi Bi.Carolina Mtuli amekiri kijiji hicho kukabiliwa na adha ya maji ambapo amesema licha ya jitihada nyingi lakini bado kijiji hicho hakijafikiwa na huduma ya upatikanaji wa mji safi na salama.