Dodoma FM

Abiria walalamika kucheleweshewa safari

7 January 2026, 12:22 pm

Picha ni stendi ya mabasi ya mabasi yaendayo mikoani .Picha na Habari leo.

Wamekuwa wakikumbana na adha ya kuchelewa kuanza safari kutokana na baadhi ya vituo vya mabasi kuathiriwa na hali ya mvua.

Na Anwary Shaban.

Baadhi ya wasafiri katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dodoma wameeleza kukumbwa na changamoto ya kuchelewa kuanza kwa safari zao, hali inayotokana na mvua zinazoendelea kunyesha pamoja na changamoto za miundombinu katika baadhi ya vituo vya mabasi.

Wakiongea na Taswira ya Habari wamesema kuwa tangu kuanza kwa mwezi Januari, wamekuwa wakikumbana na adha ya kuchelewa kuanza safari kutokana na baadhi ya vituo vya mabasi kuathiriwa na hali ya mvua kwani baadhi ya vituo miundombinu yake haijakidhi ubora hivyo mvua inaponyesha hujaa matope na kupelekea magari kushindwa kuingia na kutoka kituoni hapo.

Wamesema hali hiyo imekuwa ikiwasababishia usumbufu mkubwa ikiwemo kuchelewa kufika wanakokwenda pamoja na kuhatarisha usalama wao.

Kwa upande wake, dereva wa basi la kampuni ya Machame, Bwana Mahmodu Omary, amesema changamoto hizo ni za kawaida katika kipindi cha mvua, lakini madereva wamekuwa wakichukua tahadhari kubwa wanapokuwa barabarani ili kulinda usalama wa abiria.

Aidha amewashauri wasafiri kuanza safari mapema ili kuepuka usumbufu unaojitokeza kutokana na hali ya hewa na miundombinu isiyo rafiki.

Sauti ya kina Anwary.