Dodoma FM

Wafanyabiashara Dodoma kizimbani kwa kukaidi kulipa kodi

6 January 2026, 4:05 pm

Picha ni Afisa Sheria wa Jiji la Dodoma, Godfrey Ngazi akizungumza na waandishi wa habari. Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Ameongeza kuwa wafanyabiashara watakaokaidi kulipa kodi hizo watawajibishwa vikali kwa mujibu wa sheria.

Na Mwandishi wetu.

Halmashauri ya Jiji la Dodoma imewafikisha Mahakama ya Mwanzo Makole wafanyabiashara wote wa Jiji la Dodoma ambao wamekaidi kulipa kodi ya mabango, leseni ya biashara na ushuru wa huduma

Akizungumza na waandishi wa habari Afisa Sheria wa Jiji la Dodoma, Godfrey Ngazi amesema kuwa wafanyabiashara wote walipe kodi kwa wakati ili kuipa halmashauri nafasi ya kukamilisha miradi ya maendeleo na huduma muhimu kwa jamii.

Sauti ya Godfrey Ngazi.