Dodoma FM

Daraja jipya Mlowa laondoa kero ya usafiri kwa wananchi

5 January 2026, 4:46 pm

Wananchi wameipongeza serikali kwa kuchukua hatua ya kujenga daraja na kuwaondolea kero kubwa ya usafiri na kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Picha na Mtandao.

Ujenzi wa daraja hilo unakadiliwa kutumia zaidi ya Milioni mia tano ukiwa chini ya usimamizi wa mamlaka ya usimamizi barabara vijijini TARURA.

Na Victor Chigwada.

Kukamilika kwa daraja linalounganisha kata za Mlowa barabarani, Iringa Mvumi na Makang’wa imekuwa chanzo cha kuongeza shughuli za mawasiliano na uzalishaji kwa wananchi.

Baadhi ya wananchi wa Mlowa barabarani wamesema kuwa kabla ya kukamilika Kwa mradi huo wa daraja kukamilika wananchi walikuwa wakipoteza Mali zao kuchukuliwa na maji katika Korongo kubwa liliokuwa likikatiza katika barabara inayo unganisha maeneo hayo

Sauti za wananchi.

Aidha wameipongeza Serikali kwa jitihada za kutatua changamoto hiyo ambayo imekuwa ikiwa athiri pa kubwa shughuli za wananchi ikiwa ni pamoja na huduma ya usafirishaji

Sauti za wananchi.

Anjero Lucas Diwani wa Kata ya Mlowa Barabarani amekiri ujenzi wa daraja hilo umekuwa mkombozi Kwa wananchi wa Kata hizo tatu

Sauti ya Anjero Lucas.