Dodoma FM
Dodoma FM
24 December 2025, 3:47 pm

Maadhimisho hayo yaliambatana na utoaji wa elimu ya lishe, ushauri wa afya, pamoja na upimaji wa afya kwa watoto.
Na Anwary Shaban.
Diwani wa Kata Mnadani, Mugendi Karenge amewataka wananchi wa Mtaa wa Ndachi kuzingatia masuala ya afya na lishe bora ili kujenga jamii yenye nguvu na ustawi endelevu.
Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Afya na Lishe yaliyofanyika katika mtaa huo.
Kwa upande wake Muuguzi Kituo cha Afya Chang’ombe, Nyemo Mussa amesema ni muhimu mzazi kumpeleka mtoto kliniki kupata chanjo ya magonjwa kama vile pepopunda.
Kwa Upande wao wananchi wamesema kuwa elimu hiyo walipewa kwa kujifunza wataitumia ipasavyo na wale wazazi ambao wapo nyumbani watakwenda kuwapa elimu ya lishe.