Dodoma FM
Dodoma FM
24 December 2025, 3:17 pm

Usomaji wa vitabu kwa vijana unatajwa pia kama njia moja wapo ya kujiongezea maarifa.
Na Bennard Komba.
Ushauri umetolewa kwa vijana kuhakikisha wanaweka utaratibu wa kusoma vitabu mbalimbali ili kubadili fikra na kujiongezea maarifa yatakayowaongoza katika mafanikio.
Pamela Jerome ni kijana ambaye anasoma masomo ya uandisi katika chuo kikuu cha Dodoma na muandishi wa kitabu kinachoitwa ITS NOT YOU BUT YOUR POTENTIAL amefanya mahojiano na Taswira ya Habari na kueleza namna vitabu vinavyoweza kubadili fikra Chanya kwa vijana katika jamii.