Dodoma FM

Bidhaa zapanda bei kuelekea sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya

24 December 2025, 2:57 pm

Picha ni moja ya duka linalo uza vitu mbalimbali katika soko la Mpwapwa.Picha na Noel Steven.

Wananchi wamesema kuwa hali hiyo inachangiwa na kuchelewa kwa Mvua pamoja na miundombinu mibovu ya barabara.

Na Stephen Noel
WANANCHI wa wilaya ya Mpwapwa wamelalamikia kupanda kwa bei za vyakula na bidhaa mbalimbali huku msimu wa sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya ukikaribia.

Wakizungumza na Taswira ya habari Wananchi hao wamesema kuwa hali hiyo inachangiwa na kuchelewa kwa Mvua pamoja na miundombinu mibovu ya barabara, jambo linalosababisha ugumu wa usafirishaji wa mazao kutoka maeneo ya uzalishaji hadi sokoni.

Wananchi wameiomba Serikali na wadau husika kuchukua hatua za haraka ili kudhibiti hali hiyo na kuwapunguzia gharama za maisha, hasa katika kipindi hiki cha maandalizi ya sikukuu.

Sauti