Dodoma FM

VETA yaeleza mchango wake kwa wanafunzi wenye ulemavu

23 December 2025, 4:47 pm

Picha ni Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi VETA CPA Antony Kasore akiongea katika mkutano na waandishi wa habari.Picha na Farashuu Abdallah.

Wameweza kukuza ushiriki wa wanafunzi wenye ulemavu kwa kuwapa kipaumbele .

Na Farashuu Abdallah.

Katika jitihada za kuwezesha kundi la watu wenye mahitaji maalum kwenye fursa mbalimbali za kiuchumi chuo cha ufundi Veta Jijini Dodoma kimeeleza mchango wake kwa wanafunzi wenye ulemavu.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika makao makuu ya Veta jijini Dodoma kuhusu utoaji wa matokeo ya uchaguzi wa walioomba kujiunga na mafunzo ya Veta  kwa mwaka wa masomo 2026 Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi VETA CPA Antony Kasore amesema katika uchaguzi walioufanya wa wanafunzi watakaojiunga na masomo wameweza kukuza ushiriki wa wanafunzi wenye ulemavu kwa kuwapa kipaumbele .

Sauti ya CPA Antony Kasore .

Aidha Kasore ametoa wito kwa vijana kutumia fursa zilizotolewa na Veta waweze kuzitumia vyema na kujikimu kiuchumi.

Sauti ya CPA Antony Kasore .