Dodoma FM
Dodoma FM
23 December 2025, 4:33 pm

Wananchi nao wametakiwa kushiriki kikamilifu katika kulinda mazingira kwa kupunguza uchafuzi, kutumia nishati safi, kuhifadhi vyanzo vya maji, pamoja na kuzingatia mitindo ya maisha yenye kuimarisha afya kama lishe bora na mazoezi ya mara kwa mara.
Na Daniel Njau
Imeelezwa kuwa mtindo wa maisha na mabadiliko ya hali ya hewa unachangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la magonjwa yasiyo ya kuambukiza .
Kwa mujibu wa wizara ya Afya Magonjwa Yasiyoambukiza (NCDs) yanachangia takribani 33% ya vifo vyote nchini huku kwa takwimu za Shirika la Afya duniani (WHO) kwa mwaka 2020 zinaonesha kuwa magonjwa hayo yalichangia zaidi ya vifo milioni 41 sawa na 71% ya vifo vyote Duniani ukilinganisha na vifo milioni 57 kwa mwaka 2016 duniani.
Daktari mwanafunzi kutoka chuo kikuu cha Dodoma ndaki ya Afya Festo alloyce anasema Afya ya binadamu haiwezi kutenganishwa na mazingira anayoishi.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi wanasema mabadiliko ya mtindo wa maisha yakiwemo matumizi makubwa ya vyakula vilivyosindikwa, ukosefu wa mazoezi ya mwili, kuongezeka kwa uchafuzi wa mazingira, kumechangia kwa kiasi kikubwa kuibuka kwa magonjwa yasiyoambukiza .