Dodoma FM

Wananchi Mlebe waiangukia serikali ujenzi nyumba za wahudumu wa afya

23 December 2025, 4:18 pm

katika kuhakikisha wanapata wadau wamejaribu kuwasilisha maombi katika mfuko wa kusaidia Kaya masikini TASAF.Picha na Instagram.

Kwa mujibu wa sera ya afya ya mwaka 2007 Serikali Katika kuhakikisha kuwa wananchi wana afya bora, Serikali imeendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kutoa huduma za afya kwa kuzingatia sera na miongozo iliyopo.

Na Victor Chigwada.

Wananchi wa kijiji cha Mlebe Kata ya Msamalo Wilaya ya Chamwino wameiomba Serikali kuunga mkono ujenzi wa  nyumba za watumishi wa afya ulio anzishwa na wananchi.

Wakizungumza na Taswira ya habari wananchi hao wamesema wamejitahidi kukusanya fedha kwa nguvu zao wenyewe lakini kwa sasa wamekwama hivyo wanaiomba serikali isaidie kuwashika mkono ili kukamilisha ujenzi wa nyumba hizo.

Sauti za wananchi.

Naye mtendaji wa Kijiji Cha Mlebe Bw.simoni Aineya amesema katika kuhakikisha wanapata wadau wamejaribu kuwasilisha maombi katika mfuko wa kusaidia Kaya masikini TASAF lakini hawajapata majibu yoyote hadi sasa.

Sauti ya Bw.simoni Aineya.