Dodoma FM

Wananchi waitaka serikali kuharakisha mradi wa maji Mloda

22 December 2025, 6:07 pm

Zimekuwepo taarifa za kukamilika Kwa kisima kirefu Cha maji lakini hakuna mwendelezo wa taarifa hizo.Picha na DUWASA.

Diwani wa Kata ya Mlowa Barabarani Bw.Anjero Lucas amekiri uwepo mradi wa kisima Cha maji ambacho kimekamilika lakini bado wanasubiri usambazaji wa mabomba.

Na Victor Chigwada.

Wananchi wa Kijiji Cha Mloda Kata ya Mlowa Barabarani Wilaya ya Chamwino wameitaka Serikali kuharakisha mradi wa kisima Cha maji ili kupunguza adha ya matumizi ya maji yasiyo safi na salama .

Wakizungumza na taswira ya habari wamesema kuwa zimekuwepo taarifa za kukamilika Kwa kisima kirefu Cha maji lakini hakuna mwendelezo wa taarifa hizo hali inayopelekea wananchi kuendelea kuteseka na utafutaji wa huduma ya maji kijijini hapo na kukwamisha shughuli za Kila siku.

Sauti za wananchi.

Diwani wa Kata ya Mlowa Barabarani Bw.Anjero Lucas amekiri uwepo mradi wa kisima Cha maji ambacho kimekamilika lakini bado wanasubiri usambazaji wa mabomba.

Lucas ameongeza kuwa mkandarasi wa kusambaza maji hayo bado anakamilisha mradi wa eneo lingine ndipo arejee kusambaza maji katika Kijiji cha Mloda.

Sauti ya Bw.Anjero Lucas .