Dodoma FM
Dodoma FM
22 December 2025, 5:46 pm

Pia shule ya Msingi Mnadani ilipokea kiasi cha shillingi Milioni 90.4 kwaajili ya ujenzi wa madarasa matatu na matundu 12 ya vyoo.
Na Mariam Kasawa.
Afisa Tarafa Dodoma Mjini, Zainab Mabuye aliwataka viongozi Kanda Namba Sita kuhakikisha miradi yote inayotakiwa inakamiliki ifikapo Desemba 30 kama ilivyotakiwa.
Hayo aliyasema alipofanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya BOOST na SEQUIP katika kanda hiyo inayoundwa na Kata ya Miyuji, Mnadani, Msalato na Makutupora.
Alisema Serikali inadhamira nzuri ya kuhakikisha watoto wote wa Tanzania wanapata elimu bora hivyo ni jukumu la kila mwananchi kulinda miundombinu.
Ikumbukwe kuwa Shule ya Msingi Mpamaa ilipokea kiasi cha shillingi Milioni 197 kwaajili ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya shule.