Dodoma FM
Dodoma FM
19 December 2025, 3:56 pm

Ujasiriamali kama njia halali na yenye tija huku nidhamu ya kazi, ubunifu, na matumizi sahihi ya teknolojia vimetajwa kuwa miongoni mwa misingi muhimu.Picha na Un news.
Serikali na wadau wa maendeleo wamehimizwa kuendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wajasiriamali kwa kuboresha sera na mifumo ya kifedha, kutoa mafunzo ya ujasiriamali, pamoja na kurahisisha upatikanaji wa mitaji na masoko.
Na Daniel Njau.
Ujasiriamali umetajwa kuwa nguzo muhimu ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii, hasa katika kukuza ajira binafsi kwa wananchi.
Kupitia uanzishaji na uendelezaji wa biashara ndogondogo, za kati na hata za ubunifu wa kiteknolojia, ujasiriamali unatoa fursa kwa wananchi kujipatia kipato, kupunguza ukosefu wa ajira, na kuchochea ukuaji wa uchumi wa taifa kwa
ujumla.
Baadhi wa wananchi wameeleza kuwa kubadili mtazamo na kuchukulia ujasiriamali kama njia halali na yenye tija huku nidhamu ya kazi, ubunifu, na matumizi sahihi ya teknolojia vimetajwa kuwa miongoni mwa misingi muhimu ya mafanikio katika safari ya ujasiriamali.
Bw Mohamed Sangala mkufunzi wa ujasiriamali amesema Kupitia mchakato huu, vijana na wanawake, ambao mara nyingi hukumbwa na changamoto ya ajira rasmi, hupata nafasi ya kujiajiri na hatimaye kuajiri wengine.