Dodoma FM

Wazazi Chidachi waomba kivuko wakihofia usalama wa watoto wao

19 December 2025, 3:38 pm

Ukosefu wa kivuko umekuwepo kwa muda mrefu na imekuwa likiwaathiri zaidi wanafunzi hususani msimu wa mvua.Picha na blog.

Licha ya kuomba msaada kwa serikali juu ya kivuko hicho pia viongozi wa eneo hilo wanaendelea kuchukua hatua ili kutatua tatizo hilo.

Na Farashuu Abdallah.

Katika kuelekea msimu wa mvua mkoani Dodoma wakazi wa Mtaa wa Chidachi Kata ya Mkonze wameomba kuwekewa kivuko imara katika eneo la Shule ya Sekondari na Msingi Mkonze ili kuondoa changamoto ya kuvuka kipindi cha mvua.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Chidachi Bw. Mohamed Ramadhani amesema tatizo hilo limekuwepo kwa muda mrefu na limekuwa likiwaathiri zaidi wanafunzi hususani msimu wa mvua kwani korongo hujaa maji hali inayohatarisha usalama wao wakati wa kuvuka.

Ameongeza kuwa licha ya kuomba msaada kwa serikali juu ya kivuko hicho pia viongozi wa eneo hilo wanaendelea kuchukua hatua ili kutatua tatizo hilo huku akiwataka wananchi kuwa na subira wakati juhudi hizo zikiendelea.

sauti ya kina.