Dodoma FM
Dodoma FM
18 December 2025, 4:10 pm

Mkutano ulioitishwa ulikuwa na ajenda muhimu kama vile ardhi hivyo ni vigumu kuendesha ajenda hizo muhimu na kuchangia na mawazo ya watu wachache.
Na Victor Chigwada.
Wananchi wa mtaa wa Ihumwa A wametakiwa kuhudhuria mikutano ya mtaa ili kushiriki maamuzi ya maendeleo ya mtaa pamoja.
Hayo yana jiri baada ya mwenyekiti wa mtaa wa Ihumwa A kulazimika kuahirisha kikao cha mtaa kutokana na idadi ndogo ya watu walio fika kwenye mkutano huo.
Lameki Mbinda mwenyekiti wa mtaa huo amesema kuwa licha ya matangazo kutangazwa mataani lakini idadi ya watu walio fika hawampi kibali Cha kuendelea na mkutano huo.
Mbinda amewatia moyo wale walio fika na kuwataka wakawe wajumbe wema Kwa wengine ili wawahimize kufika kwenye mkutano mwingine utakapo tangazwa.
Mbinda ameongeza kuwa mkutano ulioitishwa ulikuwa na ajenda muhimu kama vile ardhi hivyo ni vigumu kuendesha ajenda hizo muhimu na kuchangia na mawazo ya watu wachache .
Nao baadhi ya wananchi walio fika katika mkutano huo wametoa wito Kwa jamii kubadilika na kufika katika mikutano kwani maendeleo ya mtaa yanategemea uwepo wa uhusiano mzuri wa jamii na viongozi wake.