Dodoma FM
Dodoma FM
17 December 2025, 4:47 pm

Siku 16 za kupinga ukatili huadhimishwa kila mwaka kuanzia novemba 25 hadi desemba 10 ambapo chama hicho kimeamua kuadhimisha siku hiyo mwanzoni mwa jumahili desemba 15 mwaka huu.
Na Mariam Matundu.
Chama cha ushirika cha wakulima wa Zabibu na masoko (WAZAMAM) kimeadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ili kutoa elimu ya ukatili kwa wanachama wake katika kata ya Mpunguzi jijini Dodoma.
Bakari mavula ni meneja mradi kutoka chama hicho amesema kufuatia matukio ya ukatili wa kijinsia kukithiri katika jamii wameamua kuwaalika wataalamu ili kutoa elimu hiyo ambayo imesaidia jamii kutambua haki zao.
Kwa upande wake afisa ustawi wa jamii kutoka jiji la Dodoma Anneth Mwambya amesisitiza wananchi kutumia vituo jumuishi vya kusaidia wahanga wa ukatili ONE STOP CENTER ili kupata huduma muhimu na kwa haraka kwa walio fanyiwa ukatili huku afisa sheria kutoka chama cha wanasheria wanawake Tanzania TAWLA Andrew Mhimba suala la umasikini bado linarudisha nyuma jitihada za kupambana na ukatili.
Baadhi ya wanachama cha WAZAMAM wamekiri kunufaika na elimu inayotolewa na wataalamu kila mara na kwamba imewasaidia kupasa sauti kupambana na vitendo vya ukatili.