Dodoma FM

Senyamule; Limeni mazao yanayo stahimili mvua chache

17 December 2025, 3:47 pm

Kutokana na utabiri wa uwepo wa kiwango kidogo cha mvua Mkoani Dodoma ni vyema wananchi wakalima mazao yanayoendana na hali hiyo.Picha na haicco_tanzania.

Maagizo hayo yanatokana na kauli iliyotolewa na mamlaka ya hali ya hewa Tanzania TMA hivi karibuni juu ya utabiri wa muelekeo wa msimu wa mvua za vuli na mvua za msimu kwa kipindi cha Oktoba 2025 hadi Desemba 2025 na kipindi cha mwezi Novemba, 2025 hadi Aprili 2026 mtawalia.

Na Farashuu Abdallah.
Wananchi Mkoani Dodoma wametakiwa kulima mazao yanayo stahimili ukame.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh. Rosemary Senyamule katika kikao na Maafisa ugani kilichofanyika katika ukumbi wa Safina mkoani Dodoma chenye lengo la kuazimia mazao sahihi ya kulima kulingana na badiliko ya tabia nchi.

Senyamule amesema kutokana na utabiri wa uwepo wa kiwango kidogo cha mvua Mkoani Dodoma ni vyema wananchi wakalima mazao yanayoendana na hali hiyo ili kuepuka changamoto zinazoweza kutokea hapo baadaye kama vile ukosefu wa chakula.

Sauti ya Mh. Rosemary Senyamule

Baadhi ya maafisa kilimo walio hudhuria kikao hicho wamesema maelekezo hayo waliyo pewa na Mkuu wa Mkoa yatawasaidia wao kwenda kuongeza uelewa kwa wananchi na kuwahamasisha kulima mazao yanayo stahimili ukame.

Sauti za maafisa ugani.