Dodoma FM
Dodoma FM
16 December 2025, 3:57 pm

Wakizungumza na taswira ya habari baadhi ya wachinjaji wa maeneo hayo wanasema wekuwa wakichinja mifugo yao Kwa Njia za asili.
Na Victor Chigwada.
Wananchi wa kijiji cha Mlebe Kata ya Msamalo Wilaya ya Chamwino wameiomba Serikali kuwajengea machinjio ya kisasa Ili kuongeza usalama na ufanisi wa upatikanaji wa kitoweo Cha nyama
Jambo ambalo sio salama sana kwa watumiaji kutokana na mazingira ambayo hayana maboresho na kuwalazimu kuchinja Kwa kutandika majani chini ama kuning’iniza kwenye miti.
Afisa mtendaji kijiji cha Mlebe Bw.Simoni Aineya amesema kuwa bado inahitajika fedha kwaajili ya utekelezaji wa ujenzi wa makalo ya machinjio hayo ili kuondoa uchinjaji holela ambao unafanyika Kwa sasa licha ya uwepo wa eneo la Kijiji lililotengwa kwaajili ya shughuli hiyo ya uchinjaji.
Aineya ameongeza kuwa kufanikiwa Kwa ujenzi huo italeta tija Kwa wananchi wanao jishughulisha na shughuli hizo za uchinjaji sanjali na kuongeza Pato la Kijiji kupitia ushuru wa kalo.