Dodoma FM
Dodoma FM
15 December 2025, 3:51 pm

Utunzaji wa mazingira ni muhimu katika jamii hususani utunzaji wa milima.
Na Farashuu Abdallah.
Wananchi wamehimizwa kutunza mazingira ili kuepuka athari hasi zinazoweza kutokea katika jamii.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa kitengo cha mawasiliano Serikalini halmashauri ya jiji la Dodoma Dennis Gondwe wakati akizungumza na Dodoma Fm amesema utunzaji wa mazingira ni muhimu katika jamii hususani utunzaji wa milima kwani ni chanzo kimojawapo cha kukuza uchumi wa nchi.
Aidha, Gondwe amemaliza kwa kuishauri jamii juu ya utunzaji wa mazingira ili kulinda rasilimali zilizopo.