Dodoma FM

Uhaba wa walimu chanzo cha wanafunzi kukata tamaa Igandu

15 December 2025, 3:11 pm

Hali hiyo inapelekea wanafunzi kushindwa kuelewa na masomo ya sekondari na kujikuta wengi wakikata tamaa na kuacha shule.Picha na Mtandao.

Kitendo Cha mwalimu mmoja kujigawa katika madarasa mengi inakuwa ngumu kuhakikisha kama wanafunzi wanaelewa kile wanacho fundishwa.

Na Victor Chigwada.

Uhaba wa  walimu  katika shule ya msingi Igandu umepelekea baadhi ya wanafunzi wanao maliza darasa la saba shuleni hapo kujiunga kidato cha kwanza bila kuwa na uwezo mzuri darasani.

Wakizungumza na Taswira ya habari wamesema  kuwa kitendo Cha mwalimu mmoja kujigawa katika madarasa mengi inakuwa ngumu kuhakikisha kama wanafunzi wanaelewa kile wanacho fundishwa.

Wamesema kuwa Hali hiyo inapelekea wanafunzi kushindwa kuelewa na masomo ya sekondari na kujikuta wengi wakikata tamaa na kuacha shule.

 Aidha wamesema kuwa idadi kubwa ya wanafunzi inapaswa kuendana na idadi ya walimu hususani walimu wa jinsia ya kike Ili kuwapa uhuru wa kujieleza katika hatua za ukuaji

Sauti za wazazi.

Joyce Chiloweka mwenyekiti wa Kijiji Cha Igandu anasema kuwa changamoto kubwa katika shule Yao ya msingi ni walimu licha ya kuwa na majengo ya kujitosheleza

Sauti ya Bi. Joyce Chiloweka.