Dodoma FM

Maafisa usafirishaji waitaka jamii kutowahusisha na vitendo vya uhalifu

11 December 2025, 3:44 pm

Picha ni maafisa usafirishaji katika semina iliyofanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Bogwe, Wilayani Kasulu, Kigoma. Picha na LATRA.

Hayo yanajiri kutokana na mitazamo tofauti katika jamii ikiwepo baadhi yao kuhusishwa na matukio ya kihalifu kwa kilekinachodaiwa maafisa hao kushiriki katika matukio ya uvunjifu wa amani nchini.

Na Benard Komba.

Maafisa usafirishaji jijini Dodoma wameitaka jamii kuondoa mitazamo hasi ikiwemo kuwahusisha katika matukio ya uhalifu na badala yake wawaunge mkono kutokana na sekta hiyo kuajiri idadi kubwa ya vijana nchini.

Wakizungumza na Taswira ya Habari maafisa usafirishaji wamesema kazi hiyo inatakiwa kuheshimiwa kwani imeajiri vijana wengi ambao ni wasomi.

Joseph Mjungu ni mwenyekiti wa maafisa usafirishaji katika soko la Machinga Complex Dodoma amesema sio sawa kuhusisha kazi ya bodaboda na uhalifu kwani kazi hiyo ili ifanikiwe inahitaji ukaribu na jamii pamoja na jeshi la polisi.

Sauti ya Joseph Mjungu.

Kwa upande wake Issa Rashid Makamu Mwenyekiti wa umoja wa maafisa usafirishaji mkoa wa Dodoma amesema jamii iondoe mitazamo hasi kuhusu kazi hiyo kwani imekuwa na mchango mkubwa kutokana na kuajiri vijana wengi wasomi.

Sauti ya Issa Rashid.

Biashara ya usafirishaji maarufu bodaboda ni chanzo kikubwa cha ajira kwa vijana, hasa katika maeneo ya mijini na vijijini, ikiwasaidia wengi kupata kipato nakupunguza wimbi kubwa la vijana wasionaajira.