Dodoma FM
Dodoma FM
10 December 2025, 4:56 pm

Picha ni Bi. Eliwaza Ndalu Afisa lishe halmashauri ya Mpwampwa katika kikao cha tathmini cha mkataba wa lishe ndani ya wilaya ya Mpwapwa. Picha na Steven Noel.
Bi. Ndalu amewahimiza wananchi kushirikiana na watendaji wa afya katika kufanikisha elimu ya lishe na kuhakikisha vyakula vya nyumbani vinavyotengenezwa vinajumuisha madini muhimu ili kupunguza hatari ya ugonjwa wa upungufu wa madini.
Na Steven Noel.
Jamii imetakiwa kuzingatia utumiaji wa vyakula vilivyoongezwa madini joto ili kupunguza magonjwa miongoni mwa watoto na akina mama.
Kauli hiyo imetolewa na Bi. Eliwaza Ndalu, akizungumza na watendaji wa kata katika kikao cha tathimini cha mkataba wa lishe kilichofanyika ndani ya Wilaya ya Mpwapwa.
Bi. Ndalu amesisitiza kuwa vyakula vilivyo na madini joto kama vile chuma na zinki ni muhimu kwa ukuaji na afya bora ya watoto, huku akibainisha kuwa wanawake wajawazito na wale walio katika kipindi cha unyonyeshaji wanapaswa kutilia mkazo matumizi ya vyakula hivyo.