Dodoma FM

Mkuu wa Kitengo cha Taka Jiji la Dodoma afanya ukaguzi wa usafi Makulu

10 December 2025, 4:35 pm

Picha ni Dickson Kimaro Mkuu wa Kitengo cha Usafi na Udhibiti wa taka ngumu katika ziara ya ukaguzi wa usafi wa mazingira Kata ya Dodoma Makulu. Picha na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya.

Ziara hiyo imelenga kutathmini hali ya usafi kwenye mitaa mbalimbali na kuhakikisha kuwa huduma ya uondoaji taka inatekelezwa ipasavyo.

Na Mwandishi wetu.

Mkuu wa Kitengo cha cha Usafi na Udhibiti wa taka ngumu Jiji la Dodoma, Dickson Kimaro amefanya ziara ya ukaguzi wa usafi wa mazingira pamoja na mzabuni wa huduma za ukusanyaji na uondoshaji wa taka katika Kata ya Dodoma Makulu.

Katika ziara hiyo, Kimaro na mzabuni wametembelea maeneo ya barabara kuu na mitaa yenye msongamano wa wananchi wakiangalia namna usafi unafanyika na uwepo wa taka unavyokusanywa.

Akizungumza wakati wa ukaguzi, Kimaro amesisitiza umuhimu wa kuwa na mazingira safi, akibainisha kuwa usafi ni sehemu ya kulinda afya za wananchi na kuimarisha hadhi ya kata. Aidha amemtaka mzabuni kuongeza nguvu kazi, kufuata ratiba kwa wakati, na kuhakikisha taka hazikai kwa muda mrefu katika vituo vya kukusanyia.

Kimario amehitimisha kwa kutoa wito kwa wananchi wa Dodoma Makulu kushirikiana na uongozi wa kata na mzabuni kwa kutupa taka katika maeneo rasmi, kutenganisha taka na kulinda vifaa vya usafi vilivyowekwa katika mitaa yao.

Sauti ya Dickson Kimaro.

Ziara hiyo imemalizika kwa maelekezo ya haraka ya kuboresha usafi kwenye maeneo yaliyobainika kuwa na changamoto, na kuweka ratiba ya ufuatiliaji kila wiki ili kuhakikisha jiji la Dodoma linakuwa salama na safi wakati wote.