Dodoma FM
Dodoma FM
10 December 2025, 4:12 pm

Picha ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule wakati wa hafla fupi ya utiaji saini Mkataba wa ununuzi wa Miche ya Tufaa baina ya Mkoa wa Dodoma na Kampuni ya Tamtam Tanzania ya Mkoani Iringa katika Ukumbi wa Ofisi yake Jijini humu.
Senyamule amesema kuwa mkoa wa Dodoma una lengo la kulifanya zao la tufaa kuwa kati ya mazao ya kimkakati na lenye kuinua uchumi kwa mkoa na mwananchi mmoja mmoja.
Na Mariam Kasawa.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule amewataka wananchi kupanda miche ya miti ya matunda ya tufaa kwasababu ni zao lenye tija katika kuinua uchumi wa mkoa wa Dodoma.
Ameyasema hayo katika hafla ya utiaji saini wa mkataba wa Ununuzi wa Miche ya Tufaa uliohusisha Kampuni ya Tamtam kutoka Mkoa wa Iringa na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma iliyofanyika katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Senyamule amemalizia kusema kuwa Mkoa wa Dodoma umekuwa na kampeni ya kupanda miti yenye jina la Kijanisha Dodoma ambapo utiaji wa saini wa mkataba huo utakuwa katika utekelezaji wa kampeni hiyo kwasababu matunda hujenga afya ya mwili, hutoa chakula, kuinua kipato, kutoa ajira, kuweka kivuli na kutunza mazingira.

Picha ni Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mjini Mhe. Alhaj Jabir Shekimweri wakati wa hafla fupi ya utiaji saini Mkataba wa ununuzi wa Miche ya Tufaa baina ya Mkoa wa Dodoma na Kampuni ya Tamtam Tanzania ya Mkoani Iringa .
Nae, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwa kuidhinisha zao la tufani kuwa la kimkakati kwasababu ni zao mtambuka.
Amesema kuwa ataweka msukumo na ufatiliaji wa kina katika kilimo cha zao la Tufaa ili kuhakikisha wananchi wanajitokeza na kuunga mkono lengo la kukuza uchumi wa mkoa na pato la taifa.