Dodoma FM
Dodoma FM
8 December 2025, 5:02 pm

Picha ni Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma, Mhe. Alimwoni Chaula wakati wa mkutano wa kwanza wa Baraza la Madiwani uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri. Picha na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya.
Ikumbukwe kuwa, katika uchaguzi uliofanyika hivi karibuni, Madiwani walipiga kura ambapo Bakari Fundikila alitangazwa kuwa Naibu Meya baada ya kupata kura 55, huku Alimwoni Chaula akichaguliwa kuwa Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma kwa kupata kura zote 57 zilizopigwa.
Na Lilian Leopold.
Masuala ya ardhi, afya pamoja na upatikanaji wa mikopo kwa watu wenye ulemavu, wanawake na vijana yamewekwa miongoni mwa vipaumbele vinavyotarajiwa kufanyiwa kazi na uongozi mpya wa Jiji la Dodoma, ikiwa ni sehemu ya mpango wa kuboresha huduma kwa wananchi.
Hayo yameelezwa na Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma, Mhe. Alimwoni Chaula, wakati wa mkutano wa kwanza wa Baraza la Madiwani uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri.
Kwa upande wake, Naibu Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma, Bakari Fundikila, amesema kuwa kwa kushirikiana na Meya watahakikisha wanasimamia kikamilifu utekelezaji wa malengo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, hususan katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na zinazokidhi mahitaji yao.