Dodoma FM
Dodoma FM
8 December 2025, 4:46 pm

Licha ya zahanati hiyo kuwa na wahudumu wa afya lakini bado kuna changamoto ya dawa. Picha na Mtandao.
Aidha, wananchi wameitaka serikali kuweka utaratibu wa ufuatiliaji wa mahitaji ya dawa ili kuhakikisha zahanati hiyo inakuwa na akiba ya kutosha muda wote na kuondoa adha wanayoipata kwa sasa.
Na Victor Chigwada.
Wananchi wa Kijiji cha Manchali A wameiomba serikali kuhakikisha huduma za dawa katika zahanati yao zinaboreshwa ili kuondoa malalamiko ambayo yamekuwa yakiibuka mara kwa mara pindi wanapofika kupata matibabu.
Wakizungumza na Taswira ya Habari, wananchi wamesema kuwa licha ya juhudi na kujituma kwa watoa huduma waliopo, changamoto kubwa inayowakabili ni upungufu wa dawa hali ambayo imekuwa ikidumu kwa muda mrefu.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kijiji cha Manchali A, Ndg. Manyangalazi Manyangalazi, amethibitisha kuwepo kwa zahanati hiyo ambayo kwa sasa inategemea kujitoa kwa watoa huduma waliopo. Amesema changamoto kuu inayoathiri utoaji wa huduma ni kukosekana kwa dawa za kutosha kwa ajili ya wananchi.