Dodoma FM
Dodoma FM
8 December 2025, 4:28 pm

Picha ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mhe. Alhaji Jabir Shekimweri katika mkutano wa kwanza wa Baraza la Madiwani. Picha na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya.
Shekimweri amesisitiza umuhimu wa madiwani kushirikiana na watendaji wa halmashauri katika kutekeleza miradi ya maendeleo, kuboresha huduma za kijamii na kusimamia ipasavyo matumizi ya rasilimali za umma.
Na Mwandishi wetu.
Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma wapongezwa kwa kuaminiwa na wananchi na kutakiwa kufanya kazi kwa uwajibikaji, ushirikiano na weledi wa hali ya juu.
Hayo yamesema Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mhe. Alhaji Jabir Shekimweri wakati wa mkutano wa kwanza wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma uliofanyika katika ukumbi wa halmashauri.
Aidha Shekimweri amewataka madiwani kuimarisha uwazi na uwajibikaji katika utendaji wao, kusikiliza kero za wananchi na kuhakikisha kuwa mipango ya maendeleo inalenga kuleta manufaa kwa jamii nzima.