Dodoma FM
Dodoma FM
5 December 2025, 3:49 pm

Kutokufanya ukarabati na uchongaji wa barabara ni kuwatesa wananchi ambao wanahitaji miundombinu iliyokamilika.
Na Victor Chigwada.
Diwani wa Kata ya Muungano Wilaya ya Chamwino ameiomba Serikali kuingilia kati changamoto ya miundombinu ya barabara inayo ikabili kata hiyoili kurahisha huduma za kijamii.
Akizungumzia changamoto hiyo Atanasi amesema kuwa barabara nyingi zilizopo katika kata yake ukarabati haujakamilika kutokana na eneo lao kuingiliana na Halmashauri ya Jiji la Dodoma hivyo TARULA kushindwa kuwa na matengenezo ya moja kwa moja katika barabara hizo .
Amesema kuwa kutokufanya ukarabati na uchongaji wa barabara ni kuwatesa wananchi ambao wanahitaji miundombinu iliyokamilika ili kuendesha shughuli za kiuchumi sambamba na kusafiri kiurahisi kufuata huduma muhimu.
Aidha baadhi ya wakazi wa Muungano wamesema kuwa kufunguka kwa barabara hizo itasaidia kuondoa adha kwa akina mama wajawazito pindi wanapopelekwa hospitali kujifungua.